27.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Mbassa wa Chadema afariki dunia akiwa usingizini

 Dk. Anthony Mbassa
Dk. Anthony Mbassa

Na Fredrick Katulanda, Mwanza

ALIYEKUWA Mbunge wa   Biharamulo Magharibi kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Anthony Mbassa alifariki dunia jana usiku  akiwa usingizini nyumbani kwake.

Taarifa zilizopatikana kutoka Biharamulo na kuthibitishwa na Msemaji wa familia, Pendo Ngonyani, zilieleza kuwa kifo cha Dk. Mbassa kilifahamika alfajiri ya jana.

Alisema  watoto walipokwenda kumuamsha hakuamka hali iliyowalazimu    kuwamuita mama yao ambaye aliwasiliana na madaktari wa Hospitali ya Biharamulo na kuthibitishwa kuwa alikuwa amefariki dunia.

Dk. Mbasa ambaye alikuwa mbunge   mwaka 2010 baada ya kushinda uchaguzi mkuu, hakurejea kwenye ubunge baada ya kuangushwa na mshindani wake, Oscar Mkasa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika uchaguzi mkuu wa Oktoba, 2015.

Akizungumzia kifo hicho, Pendo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha) Mkoa wa Kagera, alisema Dk. Mbassa alifariki dunia akiwa usingizini.

Pendo alisema  haijafahamika  sababu ya kifo chake ingawa familia imedokeza inataka uchunguzi ufanyike   kubaini sababu ya kifo hicho.

Kwa mujibu wa maelezo ya familia,   juzi mkewe akiwa kazini, yeye (Dk. Mbasa) alitoka na kurudi  jioni saa   12 na kuacha gari lake nyumbani na kwenda ambako   hakujajulikana.  Alirudi nyumbani   saa 5.00 usiku akiwa akionekana kuwa amelewa.

“Nimeelezwa kuwa baada ya kuacha gari alitoka kwa mguu kuanzia hiyo saa 12 na kurejea   yumbani saa 5.00 usiku.  Haijajulikana alikwenda wapi  lakini alirejea akiwa amekunywa alikuwa akihangaika na ilidhaniwa ni hali ya pombe, ndiyo hivyo asubuhi alikutwa akiwa amefariki dunia.

“Leo alikuwa na safari ya kwenda Bukoba   kuwasiliana na mawakili wake kwa ajili ya kushughulikia madai ya fidia ya  Sh milioni 60 za gharama za kesi namba 5/2010, iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea ubunge wa CCM jimbo hilo, Oscar Mkasa,” alisema.

Alisema kinachosubiriwa hivi sasa ni ndugu na jamaa   kupanga utaratibu wa maziko.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles