27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Wabunge wabaguana kwenye michezo

upinzani wasimamaNa Kulwa Mzee, Dodoma

WABUNGE wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), wameazimia kutoshirikiana na wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika michezo ya aina yoyote.

Maazimio hayo yalifikiwa jana baada ya wabunge hao kutoka ndani ya Ukumbi wa Bunge huku wakiwa wameziba midomo yao kwa plasta na karatasi nyeupe, ikiwa ni ishara kupinga kunyimwa haki za kuzungumza ndani na nje ya Bunge.

Akizungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya Bunge jana, Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea (Chadema), alisema wamefikia uamuzi huo ili kuionyesha dunia kwamba wanapinga hatua ya Serikali kuwanyima uhuru wa kuzungumza kinyume na Katiba ya nchi.

“Leo tumekubaliana hatutashiriki katika michezo na wabunge wa CCM, hilo tumeanza leo asubuhi kwenye mazoezi katika viwanja mbalimbali, hivi sasa tunatafakari hata kutafuta uwanja wetu.

“Tukikutana katika uwanja mmoja, sisi tutatumia upande mmoja na wao watatumia upande mwingine, hatuchanganyani, hata salamu leo kuna mmoja kanisalimia nimekwepesha mkono wangu,” alisema Kubenea.

Kubenea alisema hata katika mechi zinazoandaliwa kwa ajili ya timu ya wabunge Ukawa hawatashiriki katika kipindi hiki cha wiki mbili zilizobakia za bajeti.

“Si katika michezo tu, hata katika mahusiano, tumekubaliana kama kuna wabunge wana mahusiano ya kimapenzi na wabunge wa CCM yasitishwe kwa muda wa wiki mbili mpaka tutakavyoamua vinginevyo,” alisema Kubenea.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles