26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Lissu, wahariri Mawio wapandishwa kortini

Pg 2 juni 15
Mhariri wa gazeti la Mawio Simon Mkina akiwa na Ismail Mehbob ambaye ni mchapishaji katika kesi inayowakibili kuhusu gazeti hilo kudaiwa kuandikia habari za uchochezi za Zanzibar iliyotajwa jana katika mahakama ya kisutu jijini Dar es Salaam jana.Picha na John Dande

Na Patricia Kimelemeta, Dar es Salaam

MBUNGE WA Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema),   na wahariri wa gazeti lilofungiwa kwa muda usiojulikana la Mawio, wamepandishwa kizimbani wakikabiliwa na mashtaka matano.

Akisoma hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, Wakili wa upande wa Jamhuri, Paul Kadushi,  aliwataja washtakiwa wengine kuwa ni Mhariri wa gazeti hilo, Simon Mkina,   mwenzake Jabir Idrisa   na mchapishaji wa Kampuni ya Jamana, Ismail Mehboob.

Alidai  washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka matano likiwamo la kuandika habari za uchochezi kinyume na Sheria ya Magazeti ya Mwaka 2002.

Alidai     Januari 12 hadi 14, 2016 katika jiji la Dar es Salaam, washitakiwa watatu, Jabir, Mkina na Lissu, kwa pamoja waliandika na kuchapisha taarifa‎ za uchochezi zenye kichwa cha habari kisemacho, ‘Machafuko yaja Zanzibar’.

Katika shtaka la pili alidai   washatakiwa ,   Januari 14, 2016 katika jiji la Dar es Salaam,  walichapisha habari hizo ili kuleta chuki kwa wananchi wa Zanzibar.

Shtaka la  tatu linamkabili mshtakiwa wa tatu, Mehboob  ambaye anadaiwa kuwa Januari 13 katika jengo la Jamana lililopo Manispaa ya Ilala,  Dar es Salaam, alichapisha gazeti la Mawio lililokua na taarifa za uchochezi.

Alidai mshtakiwa huyo pia  alichapisha gazeti hilo bila ya kuwasilisha hati ya  sheria ya kiapo kwa Msajili wa Magazeti.

Shtaka la tano linawakabili washtakiwa wote kwa pamoja ambao wanadaiwa kuwa  Januari 14, 2016,  Dar es Salaam, bila ya kuwa na mamlaka yoyote,  waliwatisha na kuwatia hofu wananchi wa Zanzibar   wasiweze kuingia kwenye marudio ya Uchaguzi Mkuu.

Wakili huyo   alidai   upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na kuiomba mahakama  kupanga tarehe nyingine kwa ajili ya kuanza kusoma maelezo ya awali.

Vilevile, aliiomba mahakama   kutoa hati ya wito wa mahakama kwa washtakiwa wawili,   Tundu Lissu na Jabir Idrissa ambao hawakuwapo mahakamani,   waweze kufika kwenye tarehe nyingine itakayopangwa.

Upande wa utetezi  ambao ulikuwa unaongozwa na Wakili Peter Kibatala,  uliiomba mahakama  kufuta mashtaka hayo kwa sababu hayajakidhi matakwa ya  sheria.

Kibatala alidai mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi hiyo kwa sababu wahusika ni  Zanzibar na siyo Tanzania Bara.

Alisema Sheria ya Magazeti haiko kwenye Sheria ya Muungano, hivyo  mahakama hiyo inapaswa kutupilia mbali mashtaka hayo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles