25 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Niyonzima aibeza TP Mazembe

Haruna NiyonzimaNA MWALI IBRAHIM, DAR ES SALAAM

KIUNGO mahiri wa timu ya Yanga, Haruna Niyonzima, amesema haofii kukutana na TP Mazembe waliyopangwa nayo kundi moja kwenye hatua ya nane bora Kombe la Shirikisho Afrika, kwa kuwa anaifahamu vizuri.

TP Mazembe walishindwa kutetea taji la ubingwa wa Afrika mwaka huu baada ya kuondoshwa hatua ya 16 bora ya Klabu Bingwa Afrika sawa na Yanga, ambapo zote zilifanikiwa kuingia hatua ya 16 bora ya Kombe la Shirikisho na kukata tiketi ya kucheza makundi.

Yanga inatarajia kushuka dimbani Juni 17, mwaka huu kuikabili timu ya Mo Bejaia ya Algeria ugenini kabla ya kuwa mwenyeji wa TP Mazembe Juni 28, mwaka huu katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Yanga ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara na Kombe la FA msimu huu, wataingia tena uwanjani Julai 15, mwaka huu kusaka pointi tatu muhimu nyumbani watakapomenyana na Medeama ya Ghana, mechi zote zikiwa ni mzunguko wa kwanza wa hatua ya makundi.

Akizungumza na MTANZANIA jana kiungo huyo wa kimataifa kutoka Rwanda, alisema anakifahamu vizuri kikosi cha TP Mazembe ambacho akikilinganisha na timu yake ya Yanga ina uwezo mkubwa wa kuwabana na kuibuka na ushindi dhidi yao.

“Naifahamu vizuri TP Mazembe kwa kuwa nimekuwa nikiifuatilia, sio timu ya kutisha kwani hata Yanga tuna kikosi imara ambacho kinaweza kuwakabili na kuondoka na ushindi,” alisema.

Niyonzima alisema anaamini Yanga itafanya vizuri katika mechi zote watakazocheza kwenye hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho, kutokana na rekodi nzuri waliyoiweka katika msimu huu ambayo ni zaidi ya wapinzani wao.

Wachezaji wa Yanga wamepewa mapumziko ya wiki moja baada ya kutwaa ubingwa wa Kombe la FA Jumatano iliyopita.

- Advertisement -
Previous article
Next article

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles