24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Watoto 10 wafanyiwa upasuaji wa kichwa

Na Kadama Malunde, Shinyanga

WATOTO 10 waliobainika kuwa na matatizo ya vichwa vikubwa na mmoja mgongo wazi wamefanyiwa upasuaji na madaktari bingwa kutoka Taasisi ya Mifupa Moi, kati ya 35 mkoani Shinyanga.

Upasuaji huo, umefanyika  siku tatu zilizopita katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, ambapo jopo la madaktari  bingwa wakishirikiana na watalaamu wengine kutoka  Shirika la GSM Foundation.

Mbali ya upasuaji huo, watot 25 wamepewa matibabu ya kawaida.

Akizungumza baada ya kumaliza upasuaji huo, kiongozi wa jopo hilo kutoka Taasisi ya Moi, Dk. Josephat Kahamba, alisema kati ya watoto 35 wenye matatizo, 10 wamefanyiwa upasuaji na hali zao zinaendelea vizuri.

Alisema katika upasuaji huo, walikumbana na changamoto kubwa ya baadhi ya watoto matatizo yao yalikuwa yamekomaa.

“Naishauri jamii, iache kukumbatia matatizo haya, ikiona mtoto ana tatizo waende hospitali wapate tiba,”alisema.

Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela aliipongeza taasisi hiyo kwa kutoa tiba bure kwa wakazi wa mkoa huo.

Alisema wazazi wengi mkoani humo, wameshindwa kuwapatia matatibu watoto wao kutokana na kushindwa kumudu gharama za matibabu.

Alisema kutokana na tatizo  hilo, atawasiliana na wizara  husika  kuona namna ya kupeleka madaktari zdi ili watoe tiba kwani mahitaji bado ni makubwa.

Mmoja wa wazazi wenye watoto waliopatiwa tiba hiyo, Anastazia Peter aliwashukuru madaktari hao kwa kutoa tiba na kuitaka Serikali iangalie namna ya kufanya hivyo mara kwa mara.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles