27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Afeni Shakur ‘Mama 2pac’ atakumbukwa kwa mengi

afeni-shakurNA BADI MCHOMOLO

‘DEAR MAMA’ ni wimbo uliotungwa na kuimbwa na aliyekuwa mwanamuziki wa hip hop nchini Marekani, Tupac Shakur  ‘2pac’, ambaye sasa ni marehemu na aliuimba maalumu kwa mama yake mzazi, Afeni Shakur, ambaye amefariki juzi.

2pac aliimba wimbo huo kutokana na mama yake kuwa mpambanaji katika mambo mengi huku akimtunza kwa muda wote licha ya kupitia changamoto mbalimbali katika maisha yake na lengo lake kuu likiwa ni kuiweka familia yake katika maisha mazuri na kuwa maarufu duniani.

Licha ya kuwa mwanaharakati mama huyo hakupata umaarufu haraka hadi mtoto wake alipotambua anachokisaka mama yake akaja kumnyanyua kupitia wimbo huo wa ‘Dear Mama’ alioutoa mwaka 1995, ambapo alimuimba vema na kumsifia sana kiasi kwamba akajulikana na mashabiki wengi wa 2pac duniani kote kama alivyotamani awali kuwa maarufu.

Siasa na dawa za kulevya

Alipoingia katika siasa mama huyo alijiweka katika idara ya upigaji picha za matukio ya siasa, pia alikuwa wakili katika moja ya kampuni kubwa nchini humo lakini miaka ya 80, mama huyo alihusishwa na biashara ya dawa za kulevya kiasi kwamba akawa anasakwa na polisi mara kwa mara.

Hata hivyo, hali hiyo haikuwapendeza watu wake wa karibu akiwemo 2pac akaamua kuachana nayo akawa mshauri mzuri kwa mtoto wake juu ya dawa hizo za kulevya.

Ukombozi wa mtu mweusi

Baada ya muda, Afeni Shakur, aliamua kufundisha watu mbinu mbalimbali za kujikomboa kimaisha kiasi kwamba alifanikiwa kuwa na darasa kubwa lakini kutokana na kuwa mwangaikaji mkubwa wa kutokutaka kushindwa kitu aliamua kuachana na ufundishaji akaunda kundi la Panthers kwa ajili ya ukombozi wa mtu mweusi.

Masuala hayo yalimwingiza katika wakati mgumu baada ya kudaiwa kutaka kulipua kituo kimoja cha polisi jijini New York nchini Marekani na alipokamatwa aliweka wazi kwamba yupo tayari kwenda jela lakini wenzake waachwe waendelee na kundi hilo lililokuwa na lengo la kubadili jina na kujiita Fidel Castro aliyekuwa rais wa Cuba kati ya mwaka 1976 na 2008.

Akamatwa akiwa mjamzito

Afeni alikamatwa katika tukio hilo akiwa na ujauzito wa kwanza wa mtoto wake, 2pac, alikwenda jela akiwa mjamzito lakini kabla ya kujifungua aliachiwa huru akajifungua mwaka 1971 na mtoto wake kipenzi, 2pac ambaye alifariki mwaka 1996 kwa kupigwa risasi na kumuacha dada yake, Sekyiwa Shakur, aliyezaliwa miaka minne baadaye yaani mwaka 1975.

Kifo chake

Taarifa ya kusikitisha ilitolewa na familia yake kwamba mwanaharakati huyo alipoteza maisha akiwa na miaka 69, kifo chake kinadaiwa kimetokana na mshtuko wa moyo akiwa nyumbani kwake California nchini Marekani na kufariki baada ya kukimbizwa hospitalini.

Baada ya kifo chake familia hiyo ilitangaza kwamba mali zake na zile za marehemu 2pac zote zitasimamiwa na mtoto wake wa pili, Sekyiwa.

Awali Afeni alikuwa akiitwa Alice Faye Williams, alipohamia katika jiji la New York na kujiunga na harakati za Black Panther.

Mgogoro na mume wake

Mwezi mmoja kabla ya kifo chake alikuwa na mgogoro na mume wake, Gust Davis, kutokana na kutaka wagawane mali za marehemu 2pac na Afeni alikataa huku akidai talaka ili aendelee kumiliki mali hizo, atakumbukwa kwa mengi kutokana na harakati zake.

Kapumzike kwa amani, Afeni Shakur Davis.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles