29.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Kipa Geita Gold huru

NA ADAM MKWEPU, DAR ES SALAAM

KAMATI ya Rufaa ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imemwachia huru kipa wa timu ya Geita Gold Sport, Denis Richard, huku ikitupilia mbali rufaa saba zilizowasilishwa kwenye kamati hiyo baada ya kuonekana kuwa na hatia ya upangaji matokeo.

Hukumu hiyo ilitolewa jana baada ya siku chache kamati hiyo kuamua  kuzishusha  hadi Ligi Daraja la Pili  (SDL) timu zilizokuwa  kundi C ya ligi  inayodhaminiwa na StarTimes, ambazo ni Geita Gold Sport (Geita), Polisi  Tabora  (Tabora) na JKT Oljoro (Arusha)  baada ya kukutwa na hatia ya upangaji matokeo.

Kwenye uamuzi huo timu ya JKT Kanembwa ya mkoani Kigoma, ilishushwa hadi kwenye ligi ngazi ya mkoa (RCL), baada ya kushika nafasi ya mwisho katika msimamo wa kundi lake, Kundi C.

Hata hivyo, miongoni mwa rufaa nane zilizowasilishwa, zilikuwa ni ile ya Geita Gold, kocha msaidizi wa timu ya Geita Gold Sport, Choki Abeid, kipa wa Geita Gold Sport, Denis Richard Dioniz.

Pia rufaa ya Katibu wa Chama cha soka mkoani Tabora, Fatel Rhemtullah, mwamuzi kutoka mkoani Dodoma, Saleh Mang’ola, timu ya Soka ya Polisi Tabora, JKT Oljoro FC ya Arusha na Mwenyekiti wa Chama cha soka cha Mkoa wa Tabora, Yusufu Kitumbo.

Akisoma hukumu hiyo mbele ya waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Makao Makuu ya TFF, Wakili Revocutus Kuli alisema uamuzi huo ulitolewa kwa kufuata Kanuni za Nidhamu za TFF na rufaa kwa wahusika ipo wazi kupinga uamuzi uliochukuliwa juu yao.

“Kamati ilijiridhisha na kufuta uamuzi wake kwa kipa wa Geita, Richard baada ya kamati hiyo kuona kuna mapungufu ya kanuni ambapo iliishauri TFF kupunguza madaraka ya waamuzi.

“Baada ya kamati kuzipitia rufaa nyingine saba, iligundua hazikuwa na nguvu ya kufuta uamuzi uliotolewa mwanzo hivyo zitaendelea kutumikia adhabu kama kawaida,” alisema Wakili Kuli.

Wakati huo huo, mlezi wa timu ya Polisi Tabora, Ismail Rage, alisema kuwa baada ya kupokea barua ya hukumu watapeleka  malalamiko yao  Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA).

“Sisi tulihukumiwa kwa makosa mawili, moja tulishinda tukabakiwa na moja linalohusu maamuzi ambalo kimsingi tulionewa juu ya hilo kwa kuwa uamuzi ulitolewa kwa utashi na si kanuni.

“Baada ya kupewa barua ya hukumu kuna mambo tutayafanya ikiwamo kupeleka malalmiko yetu FIFA, ili kuomba yarudiwe na tutahitaji viongozi wote wa kamati wawepo,” alisema Rage.

Naye Mjumbe wa Kamati ya Nidhamu ya timu ya Geita, Salum Kurunge alisema kuwa licha ya Mbao FC kupandishwa watahakikisha haichezi Ligi Kuu, hadi hapo rufaa yao itakaposikilizwa mara ya pili na mwafaka kupatikana.

“Kesi ndio kwanza inaanza, kama TFF ilifikiri wamemaliza wajue haitakuwa rahisi kama wanavyodhani,” alisema Kurunge.

Alieleza moja ya utetezi wao waliwasilisha kwa njia ya sauti ya mmoja wa viongozi wa TFF aliyekuwa akidai rushwa.

“Walikwepa kuzungumzia jambo hili wakati ni la kweli, kuna harufu ya rushwa ndani yake hadi sasa taarifa ilishafika Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru),” alisema Kurunge.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles