27.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Lugola ampliua Balozi Sefue

sefueNa Bakari Kimwanga, Dodoma

MBUNGE wa Mwibara, Kangi Lugola (CCM) amesema aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue   alikuwa ni jipu lililojificha Ikulu.

Alisema hatua ya kutumbuliwa na Rais Dk. John Magufuli ni sahihi kwa vile  imeenzi kwa vitendo kauli ya Baba wa Taifa Mwalimu  Nyerere kuwa  Ikulu ni mahali patakatifu.

Kauli hiyo aliitoa   bungeni jana, alipokuwa akichangia mjadala wa hotuba ya bajeti ya Wizara ya Kilimo, Migugo na Uvuvi ya mwaka 2016/17 ya Sh bilioni 275.06.

Alisema pia kuwa hatua ya kuimarisha sekta ya kilimo huenda sambamba na uimarishaji wa maisha ya wakulima.

“Mheshimiwa Mwenyekiti hii ni mara yangu ya kwanza kuchangia bajeti tangu ilipoundwa Serikali ya Awamu ya Tano, kwa hali hiyo ninapenda kumpongeza Rais Magufuli kwa kumtumbua jipu aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi (Balozi Sefue).

Alimtaka Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba kuhakikisha anatumbua majipu yaliyopo katika wizara yake likiwamo  la wakulima hewa  kilimo kiweze kukua.

Lugola alisema Wizara ya Kilimo ni wizara nyeti ambayo inatakiwa kuangaliwa kwa umakini, lakini ina wakulima hewa, hivyo waziri anatakiwa kuwatumbua.

“Jimboni kwangu vocha za pembejeo zenye thamani ya  Sh milioni 46.3 zimetolewa kwa wakulima ambao hawapo.

“Kuna mmoja yupo Mwanza wamemuandika yupo kwenye jimbo langu kuwa ni mkulima wakati siyo kweli.

“Kna mwingine na mdogo wake wapo kata nyingine wamewaandikwa kwenye vocha za pembejeo, Nchemba tumbua jipu la wakulima hewa vinginevyo hatutapata mali shambani,” alisema

Akizungumzia kilimo cha pamba, alisema kuna kila sababu ya waziri huyo wa kilimo kwenda kutumbua majipu  hasa katika mbegu feki za pamba zisizoota za Quton na ambazo zimekuwa zikisababisha kushuka kwa zao hilo mwaka hadi mwaka.

“Hii kampuni ya mwekezaji ni feki na wabunge wamepiga  kelele kwenye bodi ya pamba wanamkumbatia… huyo ni jipu ikiwezekana waziri ukitoka hapa nenda ukatumbue jipu la kampuni ya Quton,” alisema Lugola

 

Mwigulu na bajeti bil 275.06/-

Awali akiwasilisha bajeti ya Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchema, aliomba   Sh bilioni 275.06  kwa ajili ya matumizi ya kawaida  na miradi ya maendeleo.

Upinzani

Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Magdalena Sakaya, alisema kwa kipindi cha mwaka wa fedha unaomalizika Bunge liliidhinisha Sh bilioni 60.373 kwa wizara ya mifugo na uvuvi (sasa ni idara) zikiwa ni fedha za matumizi ya kawaida na maendeleo, kati ya hizo Sh bilioni 19. 398 zilikuwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

Alisema taarifa ya Wizara inaonyesha   hadi kufikia Machi 31, mwaka huu,  wizara ilikuwa haijapokea hata Sh  moja kati ya Sh bilioni 19.4 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles