27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Polisi waua majambazi watatu  

Butusyo MwambeloNA PENDO FUNDISHA, MBEYA

WATU watatu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi, wameuawa kwa kupigwa risasi wakati wa majibizano ya risasi na askari polisi mkoani Mbeya.

Tukio hilo lilitokea jana katika Kijiji cha Matundas, kilichoko Wilaya ya Chunya, mkoani hapa.

Kaimu Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Mbeya, Butusyo Mwambelo, aliwaambia waandishi wa habari jana, kwamba majambazi hao waliokuwa na bunduki moja aina ya SMG yenye namba 1996 AFU 1120 na risasi 26 kwenye magazini, walifika katika Kijiji cha Matundasi kwa lengo la kufanya uhalifu.

Kwa mujibu wa Kamanda Mwambelo, majambazi hao, walilenga kufanya uhalifu  katika duka la jumla la vinywaji linalomilikiwa na mfanyabiashara aliyetambuliwa kwa jina moja la Hamis, mkazi wa kijijini hapo.

“Tukio hilo, lilitokea April 27 mwaka huu, saa mbili usiku. Kwa hiyo, baada ya majambazi hao kufika kijijini hapo, raia wema walitoa taarifa polisi na ndipo askari polisi walipofika kwenye eneo la tukio.

“Baada ya polisi kufika katika eneo hilo, majambazi hao walishtuka na kuanza kukimbia kuelekea Kijiji cha Matondo kwa kutumia pikipiki yenye namba za usajili MC 761 AFS, aina ya Sanlag, yenye rangi nyeusi.

“Walipoona askari wanawakaribia, majambazi walianza kurusha risasi ovyo hewani, jambo lililowafanya polisi nao kujibu mapigo.

“Wakati wa majibizano hayo ya risasi, jambazi mmoja aliyetambuliwa kwa jina moja la Baraka, alijeruhiwa baada ya kupigwa risasi mguuni na tumboni na kufariki dunia, lakini wenzake wanne walifanikiwa kukimbia.

“Baadaye, askari polisi walifanya msako kijijini hapo na kufanikiwa kuwaua majambazi wengine wawili huku wengine wakifanikiwa kutoroka,” alisema Kamanda Mwambelo.

Pamoja na hayo, kamanda huyo wa polisi, alivitaja baadhi ya vifaa vilivyopatikana eneo la tukio, kuwa ni bunduki moja aina ya SMG, yenye namba 1996 AFU 1120, ikiwa na risasi 27 kwenye magazine. Pia ilikamatwa pikipiki moja pamoja na panga.

Kamanda Mwambelo, alitoa wito kwa wananchi kuendelea na moyo wa kuwafichua watu wanaowatilia shaka ili waweze kudhibitiwa mapema kabla hawajafanya uhalifu.

Pia, aliwataka wananchi wafike katika Hospitali ya Wilaya ya Chunya kwa lengo la kuitambua miili ya majambazi hao kwa kuwa majina yao hayajatambulika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles