24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Taifa Stars kujipima kwa Kenya

taifastarzNA MWALI IBRAHIM, DAR ES SALAAM

TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, inatarajia kucheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Kenya ‘Harambee Stars’ utakaopigwa Mei 29, mwaka huu jijini Nairobi.

Mchezo huo ni sehemu ya maandalizi kwa timu zote ambazo zinajiandaa na mechi za kuwania kufuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa Afrika (AFCON) zitakazochezwa Juni mwaka huu.

Taifa Stars ambayo inashika nafasi ya mwisho katika kundi G linaloongozwa na Misri ikifuatiwa na Nigeria, inatarajia kurudiana na Misri Juni 4 mwaka huu katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Taarifa iliyotolewa Dar es Salaam jana na Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Baraka Kizuguto, ilieleza kuwa shirikisho hilo kwa kushirikiana na Shirikisho la Soka la Kenya (FKF),  wamekubaliana kufanyika kwa mchezo huo ili makocha waweze kupima vikosi vyao kabla ya kucheza mechi zao za Afcon.

Alisema kikosi cha Stars kinachonolewa na kocha mkuu, Charles Mkwasa, kinatarajia kuingia kambini mwezi ujao baada ya kumalizika kwa michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara ili kujiandaa na mchezo huo wa kirafiki kabla ya kuikabili Misri.

Wachezaji wanaounda kikosi cha Stars wanatoka kwenye timu zinazoshiriki Ligi Kuu huku wengi wakitoka katika klabu za Simba, Yanga na Azam.

Stars iliyokuwa imejikusanyia pointi nne katika kundi G baada ya kupata sare nyumbani dhidi ya Nigeria na kuifunga Chad ugenini, sasa inashika nafasi ya mwisho baada ya Chad kujitoa kwenye michuano ya Afcon.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles