24.5 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Mishahara hewa yaizundua Serikali

Mwigulu Nchemba
Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba

Aziza Masoud,Dar es Salaam

SERIKALI  imekabidhi majina ya taasisi na kampuni mbalimbali zilizohusika kutoa mishahara hewa  na kuisababishia Taifa hasara ya mabilioni ya fedha kwa vyombo vya usalama ili hatua stahiki za kisheria zichukuliwe.

Akizungumza mjini Dar es Salaam jana, Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Mwigulu Nchemba alisema   baada ya kupata taarifa za ubadhilifu huo   wizara iliunda timu ambayo ilifanya uchambuzi katika baadhi ya taasisi na  kugundua  tatizo  hilo ambalo lilikuwa linafanywa na viongozi wa makampuni husika.

“Wale waliokuwa wanachukua fedha na kuwalipa watumishi hewa  tumeshakabidhi majina yao katika vyombo vya usalama…siwezi kuliongelea kwa undani kwa sababu ya kuogopa kupoteza ushahidi,”alisema Mwigulu. Alisema vyombo vilivyokabidhiwa kazi hiyo  ni pamoja na Taasisi ya Kuzuia Kupambana na Rushwa (TAKUKURU)na jeshi la polisi.

Alisema ili kupambana na  ubadhilifu huo, wizara imeagiza taasisi na mashirika yote yanayolipwa na serikali kuhakikisha wafanyakazi wao wana akaunti za benki mbazo zitakuwa zinatumika kuinigiza mishahara moja kwa moja kutoa wizarani tofauti na ilivyokuwa awali ambapo fedha hizo zilikuwa zinakabidhiwa kwa kampuni.

Alisema uchambuzi huo,utasaidia kufuta majina ya malipo kwa watu waliopo katika kampuni na mashirika ambao wamefikisha umri wa kustaafu na badao wanalipwa mshahara na waliokufa. “Kuna ofisi nyingine walikuwa wanachukua pesa mpaka za watu waliofukuzwa,hatuwezi kukubali watu wanajituma wanapokea mishahara midogo wakati tunaendelea kulipa mishahara hewa.

“Tunaendelea kuwabana waajiri kabla ya tarehe kumi kila mwezi wawe wamewasilisha taarifa ya watu waliofanya kazi kwa mwezi huo na wanastahili kulipwa na tunalipa  wizara  lengo ni tujue hiyo hewa ipo wapi na kuepusha ucheleweshwaji wa mishahara haiwezekani mishahara tuwai kuutoa karibu tarehe 25 alafu watu walipwe mpaka tarehe kumi,” alisema Nchemba.

Alisema wizara imeanza kufanya uhakiki wa ndani kwa wafanyakazi wote. Alisema mpango huo, pia utahusisha watendaji wa  halmshauri  na wilaya ambapo  fedha za mishahara na mambo mengine zitakuwa zinawekwa katika tovuti ya wizara kabla hazijapaelekwa katika ofisi za mikoa kwa ajili ya malipo.

“Kwa sasa ofisi za wakuu wa mikoa zinagawa fedha kwa wilayani, lakini kuna malalamiko mengi watu wanapata mishahara midogo kwa sababu fedha zinazopatikana haziwatoshi, kwa sasa tutakuwa tunaweka cheki za halmshauri zote katika tovuti ya wizara  ili kila halmshauri ijue imepata shilingi ngapi kupunguza ubadhilifu mikoani” alisema Nchemba.

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

  1. Sitaki kuamini kuwa suala la mishahara hewa ndo lifahamike leo! Muda wote huo serikali ilikuwa wapi! Nadhani hii ni kujenga tu mazingira ya hoja ya kisiasa kwa wananchi kuelekea uchaguzi mkuu 2015.Tunataka utekelezaji kwa vitendo na sio maneno tu,haiingii akilini eti wapo watu wanafuja pesa za walipa kodi hali wananchi wananyanyasika kwa kukosa huduma muhimu,hasa huku vijijini!

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles