24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Polisi waomba ushirikiano kukabili mauaji ya albino

Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), Isaya Mngulu
Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), Isaya Mngulu

Na Waandishi Wetu, Dar es Salaam

MKURUGENZI wa Makosa ya Jinai (DCI), Isaya Mngulu, amesema  vitendo vya mauaji ya  albino vimeanza kushamiri tena katika baadhi ya maeneo   nchini.

Amesema  kutokana na hali hiyo, jeshi la polisi limewaomba wananchi, asasi za raia, viongozi wa dini na wanasiasa kushirikiana nao  waweze kukamata mtandao wa watu wanaojihusisha na shughuli hizo na kuwachukulia hatua.

Alisema kuwa vitendo hivyo vinahusishwa moja kwa moja na imani za ushirikina hali inayosababisha baadhi ya albino kuuawa na wengine kukatwa viungo vya mwili wao.

“Vitendo hivi vimeanza kurudi tena   nchini baada ya kudhibitiwa   kipindi kilichopita. Hii inatokana na baadhi ya wananchi kuweka mbele imani za ushirikina na kuamua kuingia kwenye mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi,”alisema Mngulu.

Alisema  jeshi la polisi linaendelea na operesheni ya kuwakamata watu wanaohusika na vitendo hivyo  waweze kuchukuliwa hatua za sheria ikiwa ni pamoja na kuwafikisha mahakamani.

Alisema kutokana na hali hiyo watu saba wamekamatwa katika tukio lililotokea Mei 12 mwaka huu mkoani Simiyu na   baadhi yao tayari wamefikishwa mahakamani.

Alisema tukio la pili lilitokea Agosti 5 mwaka huu katika Wilaya ya Kaliua mkoani Tabora ambako mtu mmoja alikatwa mkono na hadi sasa watu watatu wamekamatwa na kufikishwa mahakamani.

“Tukio la mwisho lilitokea Agosti 16 mwaka huu wilayani Igunga  ambako  mtu mmoja alikatwa mkono na watu wasiojulikana na mpaka sasa tunawashikilia watu watatu,”alisema Mngulu.

Kamanda amewaomba wananchi kupiga simu namba 0755,785,557 za makao makuu ya polisi kwa ushirikiano zaidi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles