26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Upendo Nkone naye achomoza Tamasha la Pasaka

Upendo NkoneNA MWANDISHI WETU

MWIMBAJI nguli wa nyimbo za Injili hapa nchini, Upendo Nkone, amethibitisha kushiriki Tamasha la Pasaka linalotarajiwa kufanyika Machi mwaka huu, katika mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi, Alex Msama, amesema Nkone ameungana na Rose Muhando na Bonny Mwaitege, waliothibitisha kushiriki tamasha hilo.

Msama alisema hivi sasa kamati yake inaendelea na mchakato wa maandalizi ya tamasha hilo ambalo linatarajiwa kuanzia Geita Machi 26, Mwanza (Machi 27) na Kahama (Machi 28).

“Tunaendelea na mchakato wa kufanikisha Tamasha la Pasaka 2016, lenye lengo la kusaidia wenye uhitaji pamoja na kupinga mauaji ya walemavu wa ngozi ‘albino’,” alisema Msama.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles