27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

DPP ateuliwa kuwa jaji

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Dk. Eliezer Feleshi
Aliyekuwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Dk. Eliezer Feleshi

NA AZIZA MASOUD, DAR ES SALAAM

RAIS Jakaya Kikwete leo anatarajia kuwaapisha majaji wapya wa Mahakama Kuu, akiwamo Dk. Eliezer Feleshi ambaye awali alikuwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).

Uteuzi huo umewajumuisha watumishi wa mahakama na mawakili wa Serikali wa kujitegemea pamoja na watumishi wa taasisi mbalimbali za serikali.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) juzi, inaeleza kuwa uteuzi huo umefanywa baada ya Rais Kikwete kushauriana na Tume ya Utumishi wa Mahakama.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, uteuzi huo umeanza Agosti 13, mwaka huu na wateuliwa wote wataapishwa leo saa 5:00 asubuhi katika viwanja vya Ikulu, Dar es Salaam.

Watumishi wa mahakama walioteuliwa ni Penterine Kente ambaye kabla ya uteuzi alikuwa Msajili wa Mahakama ya Rufani, Dar es Salaam, Benedict  Mwingwa aliyekuwa Msajili wa Mahakama Kuu Dar es Salaam na Edson Mkasimongwa ambaye awali alikuwa Katibu wa Jaji Mkuu.

Wengine ni David Mrango aliyekuwa Msajili Baraza la Ushindani, Dar es Salaam, Mohamed Rashid Gwae aliyekuwa Msajili Mahakama Kuu, Kitengo cha Kazi, Dar es Salaam, Dk. John Ruhangisa ambaye kabla alikuwa Msajili Mahakama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Arusha na Firmin  Matogoro aliyekuwa Naibu Mwenyekiti Baraza la Rufaa la Kodi, Dar es Salaam.

Mawakili wa Serikali na taasisi mbalimbali za serikali ni pamoja na Dk. Feleshi ambaye kabla ya uteuzi alikuwa Mkurugenzi wa Mashtaka, Dar es Salaam, Barke Mbaraka Aboud Sehel ambaye alikuwa Kaimu Mkurugenzi Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dar es Salaam.

Wengine ni Winfrida Beatrice Korosso aliyekuwa Katibu Mtendaji Tume ya Kurekebisha Sheria, Dar es Salaam, Lilian Mashaka ambaye kabla ya uteuzi alikuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, (Takukuru), Dar es Salaam.

Uteuzi huo pia umewajumuisha Leila Edith Mgonya ambaye alikuwa Msaidizi wa Waziri Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Dar es Salaam, Awadhi Mohamed aliyekuwa Mchunguzi Mkuu Takukuru, Dar es Salaam.

Kwa upande wa mawakili wa kujitegemea, walioteuliwa ni Lugano  mwandambo kutoka REX Attorneys, Dar es Salaam, Amour Khamisi  kutoka AKSA Attorneys, Dar es Salaam.

Wengine ni Paul Kihwelu aliyekuwa wakili wa kujitegemea na Mhadhiri Mwandamizi, Chuo Kikuu Huria (OUT) Dar es Salaam, Rose Ebrahimu ambaye alikuwa wakili wa kujitegemea, Bulyankulu Gold Mine Ltd, Shinyanga na Salma Maghimbi, ambaye kabla ya uteuzi alikuwa Mjumbe, Tume ya Ushindani, (FCC), Dar es Salaam.

Uteuzi huo pia umewahusisha watumishi wa vyuo vikuu, akiwamo Dk. Mary Caroline Levira, ambaye alikuwa Kaimu Mkuu wa Kitivo cha Sheria, Chuo Kikuu Kishiriki cha Ruaha na  Modesta Opiyo Makopolo aliyekuwa Mkuu wa Kitivo cha Sheria, Chuo Kikuu, Mzumbe, Morogoro.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles