24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Ndugu ataka 50 kwa 50  wanawake

Na RAMADHAN HASSAN-DODOMA

SPIKA wa Bunge, Job Ndugai amewapigia chapuo wanawake kwa kutaka wawe 50 -50 na wanaume katika nafasi za uamuzi.

Kauli hiyo aliitoa jijini  hapa jana, wakati akitangaza  semina  ya wajumbe wa Chama cha Wabunge Wanawake wa Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika, inayotarajiwa kufanyika Arusha kuanzia keshokutwa.

Semina hiyo itahusu  masuala mbalimbali yanayohusu wanawake hususan katika eneo la uchaguzi.

Spika Ndugai alikuwa akijibu maswali ya waandishi ambao walitaka kujua ni kwa kiwango gani  wanawake wapo katika vyombo vya uamuzi

Alisema kuna haja ya wanawake kuzidi kugombea nafasi mbalimbali ambapo alidai sasa kwa upande wa wabunge wanawake ni asilimia 36.6 huku kwa madiwani wakiwa ni asilimia 30 hivyo kuna haja ya kuhakikisha wanafikia 50 kwa 50 katika ngazi ya uamuzi.

“Kama mnavyojua kwa upande wa Tanzania,  madiwani wanawake wapo  asilimia 30 kwenda juu, hapa bungeni tuna asilimia 36.6 ya wabunge wote ni wanawake.

“Ije ifike mahali iwe 50 kwa 50 ili lengo kadri tunavyoeenda na tutafurahi zaidi tukifika 50 kwa 50 kwa wabunge wa kuchaguliwa moja kwa moja na wananchi kuliko njia zingine ambazo zipo.

Alisema kwa upande wa Baraza la Mawaziri kwa sasa kuna mawaziri wanawake 11 kati ya 45 na majaji ni 19 kati ya 88.

“ ‘Rafly’ kwa upande wa mawaziri kwa sasa kuna mawaziri 11 kati ya 45 na majaji ni 19 katika 88 ni wanawake na  kuwa na wabunge wengi wanawake Tanzania tupo juu,  ni  nchi ya Rwanda ndio ipo mbele.Lakini  hatujafikia pale ambapo tunatakiwa,”alisema.

Alisema katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa, unaotarajia kufanyika  Novemba 24, mwaka huu kuna haja ya wananchi kuwapa nafasi kubwa wanawake.

“Tunaposema chaguzi ,tunasema zote wapewe nafasi wanawake lakini pia tunaangalia na uchaguzi wa Serikali za mitaa, tunategemea siku moja Rais wa Yanga awe mwanamke Simba itasubiri kidogo,”alisema Ndugai huku akicheka.

Katika hatua nyingine, Spika Ndugai alisema  Makamu  wa Rais,Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika semina hiyo.

“Tunatarajia wageni mbalimbali katika siku hiyo wakiwemo,Spika wa Bunge la Afrika Mashariki, mabalozi wa nchi 17 ambazo ni wanachama,Balozi wa Uingereza nchini na yule wa Pakistan, mawaziri  na viongozi mbalimbali wanawake,” alisema  Ndugai,

mwisho

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles