24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

JENERALI MWAMUNYANGE AKABIDHIWA KERO ZA MAJI

Na TUNU NASSOR-DAR ES SALAAM


WAZIRI wa Maji na Umwagiiaji Profesa Makame Mbarawa amesema hajaridhishwa na utendaji kazi wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (Dawasa) na Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es Salaam(Dawasco).

Alitoa juzi katika uzinduzi wa bodi mpya ya Dawasa itakayoongozwa na Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange.

Dawasa na Dawsasco zipo katika mchakato wa kuunganishwa na tayari Bodi ya Wakurungezi imeteuliwa ikiongozwa na Jenerali Mstaafu Mwamunyange.

Akizungumza katika uzinduzi wa bodi hiyo mwishoni mwa wiki  Dar es Salaam, Profesa Mbarawa alimkabidhi mwenyekiti huyo mpya baadhi ya changamoto alizoziona katika muda mfupi wa uongozi katika wizara hiyo.

Alisema changamoto ziliyopo katika taasisi zote mbili za Dawasa na Dawsasco ni kushindwa kusimamia miradi ya maji na kutokukusanya mapato ipasavyo.

“Kuteuliwa kwenu kunatokana na sifa mlizonazo hivyo ninaomba mkaziangalie changamoto hizi kwa makini na kuzifanyia kazi kwa vitendo,” alisema Profesa Mbarawa.

Alisema  kwa upande wa Dawasco changamoto iliyopo ni usimamizi wa maji yanayozalishwa na ukusanyaji wa mapato.

“Mtendaji Mkuu wa Dawasco haendi kuwatembelea wateja hasa wakubwa na kutafuta wateja wengine wapya,” alisema Profesa Mbarawa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles