24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Wasafirishaji mirungi wajigeuza wanafunzi

Askari Polisi wa Mkoa wa Kilimanjaro wakitoa vifurushi vya dawa za kulevya aina ya mirungi iliyokutwa imehifadhiwa kwenye mabegi yanayotumiwa na wanafunzi baada ya kukamatwa eneo la Latina wilayani Hai juzi.

MWANDISHI WETU-MOSHI

WAFANYABIASHARA na wasafirishaji wa  mirungi wameibuka na mbinu nyingine mpya ya kujigeuza wanafunzi na   kuficha mirungi katika mikoba midogo inayotumiwa na wanafunzi kuhifadhi madaftari kwa lengo la kukwepa mkono wa polisi.

Mbinu nyingine ambazo Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro iibaini hivi karibuni ni pamoja na kutumia magari ya  fahari yakiwamo Toyota Land Cruser, Toyota Alphasad, Toyota Vanguard    na kufanyia mabadiliko gari   ya Toyota Noah  kurahisisha ubebaji wa mirungi kwa kificho.

 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi, Hamis Issah, alisema wasafirishaji wa   mirungi wameendelea kubuni mbinu kila kukicha baada ya zile za awali kushtukiwa na polisi.

Alitoa a onyo kwa wamiliki wa magari ya abiria kutojiingiza katika mtego wa kusafirisha dawa hizo.

“Hapa kuna mizigo ambayo imekamatwa na askari wetu wakiwa barabarani, hii ni mbinu mpya  ya usafirishaji.

“Hii mikoba  unayoiona yote ni inaonyesha mbebaji amebeba madaftari  anaenda shuleni.

“Lakini haya siyo madaftari ni mirungi  ni mizigo iliyokamatwa kwenye mabasi tofauti tofauti,” alisema Kamanda Issah.

Alisema katika tukio hilo watuhumiwa tisa  wakiwamo wanawake wawili wamekamatwa wakiwa na   kilogramu 64 baada ya   polisi kupekuwa magari matatu ya abiria yaliyokuwa yakitokea yakiendelea na safari kutoka Moshi kwenda Arusha.

“Naona mbinu zinaendelea kubadilika ndani ya wiki mbili, mbinu tatu tofauti, kwanza ya kujaza kwenye magari, pili ya kutoboa magari.

“Tatu kama mwanafunzi  nyingine kama mtu anaenda hospitali amejifunga maplasta sasa hizi mbinu zitafika mpaka lini na sisi tunashukuru askari wangu wanafanya kazi vizuri,” alisema.

Kamanda Issah aliwataja wanaoshikiliwa hadi sasa kuwa ni    Ibrahim Masuli, Godfrey Richard, Chrispin  Baltazar, Fanuel Hamad na Jackline Mushi.

Wengine wakiwa ni Lucy Petro , Nuru Haruna, Silvesta Fabian na Minyari Miandei.

Alisema kwa sasa apolisi wameamua kupekuwa magari yote yakiwamo ya abiria huku akiwataka abiria kutoa ushirikiano kwa polisi   wanapoona mizigo yenye  shaka ili kuwaondolea adha ya kuchelewa kufika safari zao kutokana na usumbufu watakaopata barabarani.

“Tunawasihi abiria maana kuna abiria wengine wakiona askari   wanapekua gari wanakasirika, msikasirike hii ndiyo kazi ya kupekuwa.

“Vinginevyo  muwe mnatuambia ndani ya gari amepanda mtu wa ajabu na amebeba madawa ya kulevya   ya mirungi  hapo ndiyo itakuwa ni na nafuu na tutafanya kazi kwa muda mfupi muendelee na safari,” alisema.

  Issah aliwataka wamiliki wa mabasi ya abiria kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi    kuhakikisha biashara hiyo inakoma kwa kukataa kubeba abiria wenye mizigo ambayo wanatilia shaka.

Alisema kuendelea kuwabeba kutasababisha  kuwaingiza katika matatizo na vyombo vyao.

“Kuna watu wakiona gari inapekuliwa wanatubeza.

“Hivi sasa  tukikuona wewe unatubeza askari watakukamata …  wanawabeza askari wanaofanya kazi yao  halafu tutakuhoji unatubeza kwa sababu gani.

“Kwa hali kama hiyo tunaagiza askari waendelee kukamata mirungi na wasiiache,” alisistiza.

Kukamatwa kwa dawa hizo  kunafanya idadi kamili ya    mirungi ailiyokamatwa katika   wiki mbili kufikia kilogramu 564 pamoja na vyombo vya usafiri yakiwamo magari matatu na pikipiki moja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles