27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

TFDA yaeleza madhara ya sumukuvu

NATHAN LIMU

-SINGIDA

MAMLAKA ya Chakula na Dawa (TFDA) Kanda ya Kati imetoa elimu kwa zaidi ya wanafunzi 12,000 na walimu 390 wa shule 30 za sekondari wilayani Singida kuhusu  madhara yatokanayo na vyakula vyenye sumukuvu.

Pia elimu hiyo ilihusu dawa na vipondozi vilivyopigwa marufuku kwa mujibu wa sheria vifungu namba 87 (i) na 90 vya mwaka 2003.

Ofisa Elimu kwa Umma wa TFD Kanda ya Kati, Abel Daulena alisema juzi kuwa wamelega kutoa elimu hiyo kwa wanafunzi wa shule za sekondari, ambao wana uwezo wa kujitambua kama sehemu ya kudhibiti  matumizi ya vyakula vyenye sumukuvu, vipodozi na dawa zilizopingwa marufuku. 

Akifafanua zaidi, Daulena alisema wanafunzi waliopo shule za sekondari ni kizazi kinachokua, hivyo ni ukweli usiopingika kwamba kati yao wapo ambao tayari wameanza kutumia dawa na vipodozi vilivyopigwa marufuku. 

Alisema wanaamini wanafunzi hao wakitambua madhara yatokanayo na bidhaa hizo zilizopigwa marufuku, wataacha kuzitumia na pia watakuwa mabalozi wazuri kusambaza elimu hiyo kwa familia zao, na jamii inayowazunguka. 

“Mamlaka ya TFDA inafanya kila jitihada kuelimisha jamii wakiwemo wanafunzi wa shule za sekondari, kuhusu madhara mbalimbali yatokanayo na matumizi ya vipodozi vyenye viambata vyenye sumu, ili waweze kutambua na kufanya maamuzi sahihi wakati wa kununua na kutumia vipodozi hivyo,” alisema. 

Daulena ambaye pia ni mkaguzi wa chakula, vipodozi na dawa, alisema dawa zilizopigwa marufuku ni pamoja na zile za kuongeza ukubwa wa makalio na maziwa/matiti. Dawa hizo zinasadikiwa kuleta madhara kwa watumiaji, ikiwa ni kusababisha kupata ugonjwa wa saratani. 

Kuhusu vyakula visivyofaa kwa matumizi ya binadamu, ofisa huyo alisema mazao ya mahindi na karanga yanayoshambuliwa na fangasi, huzalisha sumukuvu ambayo huathiri usalama wa chakula. 

“Ulaji wa chakula kilichochafuliwa na kiasi kikubwa cha sumukuvu husababisha madhara ya kiafya na hata kifo. Madhara hayo huweza kujitokeza baada ya muda mfupi au mrefu kutegemea na kiasi cha sumukuvu kwenye chakula kilicholiwa,” alifafanua Daulena.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles