24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Salum Mayanga akabidhiwa Mbao FC hadi mwisho wa msimu

Damian Masyenene, Mwanza

Uongozi wa timu ya Mbao FC yenye maskani yake mtaa wa Sabasaba wilayani Ilemela, mkoani Mwanza, umeingia makubaliano na Salum Mayanga kuwa Kocha wake mkuu hadi mwishoni mwa msimu wa Ligi kuu bara

Mbao FC imeingia makubaliano na Mayanga ambaye anachukua mikoba ya Ally Bushiri aliyefungashiwa virago baada ya timu hiyo kutopata matokeo mazuri.

Mayanga ambaye amewahi kuifundisha timu ya Mtibwa Sugar na Taifa Stars amekabidhiwa timu hiyo ili aiwezeshe imalize katika nafasi za juu isishuke daraja.

Mayanga ni Kocha wa tatu kwa timu hiyo kwa msimu huu, ambapo mwanzoni mwa msimu ilikuwa ikifundishwa na Amri Said ambaye kwa sasa anainoa Biashara United ya Mara na baadaye ikanolewa na Ally Bushiri kabla ya Mayanga.

&&&

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles