30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Man City waweka rekodi Kombe la Carabao

MANCHESTER, ENGLAND

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu England, Manchester City, wameweka rekodi kwenye michuano ya Kombe la Carabao baada ya kuwafunga wapinzani wao, Burton Albion mabao 9-0 kwenye nusu fainali ya kwanza juzi.

Mchezo huo ulipigwa kwenye uwanja wa Etihad, huku kikosi cha Pep Guardiola kikifunga idadi kubwa ya mabao ambayo hayajawahi kufungwa kwenye hatua hiyo.

Kiungo wa Manchester City, Kevin De Bruyne, ambaye amekuwa benchi wiki kadhaa zilizopita, alikuwa wa kwanza kufungua ukurasa wa mabao katika dakika ya tano.

Hata hivyo, mshambuliaji wa timu hiyo raia wa nchini Brazil, Gabriel Jesus, alikuwa kwenye ubora wake huku akipachika mabao manne peke yake na mabao mengine yakifungwa na Oleksandr Zinchenko, Phil Foden, Kyle Walker na mshambuliaji wa pembeni, Riyad Mahrez.

Idadi hiyo ya mabao iliwahi kufungwa kwenye nusu fainali ya michuano ya Kombe la FA katika msimu wa 1871-72. Mwishoni mwa wiki iliyopita Manchester City waliwafunga Rotherham mabao 7-0 kwenye michuano ya Kombe la FA katika mzunguko wa tatu.

Idadi ya mabao ambayo imefungwa na Manchester City inaifanya klabu hiyo kuwa ya kwanza kufunga mabao mengi ndani ya England kwa kipindi cha zaidi ya miaka 51 katika michezo miwili mfululizo.

Klabu ya Leeds United ambayo ilikuwa chini ya kocha Don Revie, iliwahi kushinda mabao 9-0 dhidi ya Spora Luxembourg, Oktoba 1967, kabla ya kuja kushinda mabao 7-0 dhidi ya Chelsea.

Huo ni ushindi wa pili mkubwa kwa Guardiola akiwa kocha, aliwahi kupata matokeo kama hayo akiwa na kikosi cha Barcelona ambapo alishinda mabao 9-0 dhidi ya L’Hospitalet kwenye michuano ya Copa del Rey, Decemba 2011.

Hata hivyo, ushindi huo wa juzi kwa Manchester City ulikuwa wa kwanza kwa kushinda mabao tisa tangu walipofanya hivyo Novemba 1987, waliposhinda mabao 10-1 dhidi ya Huddersfield Town.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles