24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Maduro ashinikizwa kung’oka madarakani

CARACAS, VENEZUELA

KIONGOZI wa upinzani nchini Venezuela anayeungwa mkono na nchi za Marekani na Bunge la Umoja wa Ulaya, Juan Guaido ameongeza shinikizo dhidi ya utawala wa Rais Nicolas Maduro wa Venezuela kwa kuitisha maandamano makubwa ya umma leo kutaka kufanyika chaguzi za mapema huku Marekani ikimuonya Maduro kuwa muda umekwisha wa kufanya mazungumzo.

Nchini za Uingereza, Ufaransa, Ujerumani na Uhispania zilikuwa zimeweka muda wa mwisho wa Maduro kuitisha chaguzi mpya kuwa jana, la sivyo zitajiunga na Marekani kumtambua Guaido kuwa rais wa muda wa Venezuela.

Bunge la Umoja wa Ulaya wiki hii lilimtambua Guaido kuwa kiongozi wa muda wa Venezuela.

Maandamano ya jana yalisadifiana na sherehe za chama tawala cha Kisosholisti za kuadhimisha miaka ishirini tangu aliyekuwa rais wa Venezuela Hugo Chavez kuingia madarakani.

Katika barua aliyowaandikia marais wa Mexico na Uruguay, Guaido amesema hakuna uwezekano wa kufanya mazungumzo na Maduro hadi pale mchakato wa kuwepo serikali ya mpito utakaopelekea kuandaliwa kwa chaguzi huu utakapoanza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles