23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Maandamano kutikisa Venezuela


CARACAS, VENEZUELA

MAELFU ya wananchi wa Venezuela jana wanatarajiwa kuandamana wakati ambao kiongozi wa upinzani Juan Guaido akiendelea kumshinikiza rais Nicolas Maduro kuondoka madarakani, huku kukiendelea kukosekana huduma muhimu ya umeme, katika taifa hilo linalokumbwa na mgogoro.

Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari kutoka nchini humo zimesema kuwa Juan Guaido na Maduro ambao wote wanagombania madaraka ya kuliongoza taifa hilo la Amerika ya kusini tajiri kwa mafuta, wamewataka wafuasi wao kuandamana mjini Caracas pamoja na miji mingine.

Guaido aliandika katika mtandao wake wa kijamii wa twitter akiwataka wafuasi wake kuandamana dhidi ya Maduro kupinga utawala uliojaa rushwa na ulioitumbukiza Venezuela katika kiza.

Guaido mwenye umri wa miaka 35 anatambuliwa na mataifa zaidi ya 50 kama rais wa mpito wa Venezuela. Kwa upande wake rais wa Venezuela Nicolas Maduro amewataka wafuasi wake kuandamana dhidi ya ubeberu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles