27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Kizimbani kwa kukutwa na pombe haramu

AVELINE KITOMARY Na MARRY NYARI -DAR ES SALAAM

MKAZI wa Dar es Salaam, Chacha Marwa (32), amepandishwa kizimbani katika Mahakama ua Hakimu Mkazi Kinondoni kwa tuhuma za kukutwa na pombe haramu ya gongo yenye ujazo wa lita 160.

Akisomewa shtaka hilo mbele ya hakimu Hanifa Mwingira, mwendesha mashtaka wa Jamhuri, Matarasa Hamisi, alisema mshtakiwa huyo anadaiwa kutenda kosa hilo Novemba 10, 2018 eneo la Mabibo Jeshini wilayani Ubungo ambako alikutwa na pombe hiyo haramu jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

Mshtakiwa alikana kutenda kosa hilo na Hakimu Mwingira alisema dhamana iko wazi kwa kuwa na wadhamini wawili watakaotoa bondi ya Sh milioni moja.

Hata hivyo mshtakiwa alishindwa kukidhi masharti ya dhamana na kurudishwa rumande hadi Februari 19, mwaka huu kesi hiyo itakaposomwa tena.

Wakati huo huo, Josephat Mkombachepa (49), mkazi wa Mabibo Kisimani, amepandishwa kizimbani kwa shtaka la kujipatia fedha kwa udanganyifu.

Akisomewa shtaka hilo mbele ya Hakimu Godfrey Isaya, mwendesha mashtaka wa Jamhuri, Clara Charwe, alidai kuwa mnamo Oktoba 10, 2017 eneo la Mwananyamala,  Wilaya ya Kinondoni, mshtakiwa alipokea kiasi cha Sh 2,600,000 kutoka kwa Francis Maigwa kwa njia ya uongo.

Mshtakiwa alikana kutenda kosa hilo hivyo alirudishwa rumande hadi kesi yake itakaposomwa tena Februari 19, mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles