24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Jengeni utamaduni kuchangia afya- Dk. Mahiga

Na TUNU NASSOR-DAR ES SALAAM

WAZIRI wa Katiba na Sheria, Dk. Augustine Mahiga, amewataka Watanzania kujenga utamaduni wa kuchangia  gharama za matibabu kwa wagonjwa wasio na uwezo ili kunusuru maisha yao.

Akizungumza Dar es Salaam jana, wakati wa ufunguzi wa mbio za riadha za Heart Marathon 2019, Dk. Mahiga alisema matibabu ya magonjwa hasa ya moyo yana gharama kubwa hivyo baadhi kushindwa kumudu.

Alisema lengo la mbio hizo ni kuchangia matibabu ya watoto zaidi ya 200 waliopo katika orodha ya upasuaji wa matibabu ya moyo katika Taasisi ya Jakaya Kikwete (JKCI) lakini bado kuna idadi kubwa ambao wataendelea kusubiri kupata fedha za kugharamia matibabu yao.

“Lengo kubwa la kushiriki mbio hizi ni kwa ajili ya kuchangia fedha za kuwatibu watoto wetu pale JKCI kwa kuwa matibabu hayo ni gharama kubwa wengi wa wazazi hawamudu gharama hizi hivyo nitoe wito kwa jamii kujenga utamaduni wa kuchangia matibabu,” alisema Mahiga.

Mahiga aliitaka jamii kushiriki mazoezi mbalimbali ili kujenga mwili na kupunguza maradhi ambayo yanazuilika kwa njia hiyo.

Washindi na washiriki wa mbio hizo endeleeni kushiriki riadha kila wakati kwa kuendeleza vipaji vyenu na kuweka mwili yenu,” alisema Mahiga.

Naye Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, alisema kuna watoto zaidi ya 200 wanasubiri kupatiwa matibabu ya moyo katika taasisi hivyo jamii ishirikiane na JKCI kuwasaidia kupata matibabu .

Alisema taasisi hiyo, itaendelea kushirikiana na wadau wengine wanaokuwa tayari katika kuchangia matibabu hayo kwa ajili ya kuokoa maisha ya watoto nchini.

Kwa upande wake  Mkurugenzi wa Taasisi ya JKCI, Professa Mohamed  Janabi, alisema fedha zinazohitajika ni takribani sh milioni 200 kwa watoto 200 pekee wanaotakiwa kufanyiwa matibabu ya Moyo huku watoto wengine  512 wakiwa wanasubiri matibabu hayo.

Alisema wadai wakichangia kiasi hicho kilichobakia serikali itagharamia matibabu ya watoto bao.

“Rai yangu kwa wadau kwa kuwa maradhi haya ya moyo ni makubwa mnapotoka hapa mle kwa wastani na kufanya mazoezi ya kukimbia kusudi kuepuka maradhi haya,” alisema professa Janabi.

Naye Mkuu wa Kitengo cha Mazingira kutoka Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (Dawasa),  Mhandisi Modesta Mushi, ambaye alishiriki mbio hizo za kilomita 10, pamoja na kuchangia damu, alisema watoto hao ni sehemu ya jamii hivyo Dawasa watajitoa kuokoa maisha yao.

“Dawasa tumeshiriki kama wadau na wazazi katika ngazi ya familia, nimeona kuna umuhimu mkubwa wa kuchangia damu kwa kuwasaidia waliopo vitandani huko Hospitali,” alisema Modester.

Aliongeza kuwa watoto nao ni sehemu ya jamii na viumbe hai hivyo aliwaomba washiriki wengine kujitoa kwa ajili ya kuokoa uhai wa watoto na watu wazima.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles