30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Gbagbo akubali masharti ya ICC

THE HAGUE, UHOLANZI

ALIYEKUWA Rais wa Ivory Coast, Laurent Gbagbo amekubali masharti yaliyowekwa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC kabla ya kuachiliwa huru na majaji wa Mahakama hiyo inayoshughulikia kesi za uhalifu wa kivita ya ICC hapo.

Gbagbo amekubali masharti hayo juzi kwamba atatakiwa kuishi katika nchi ambayo itakubali kumpa hifadhi na kurejea katika mahakama hiyo iwapo atahitajika kufanya hivyo wakati wowote.

Akitangaza uamuzi huo, Jaji Chile Eboe Osuji kwa niaba ya jopo la majai watano wa ICC ameagiza kuwa Gbagbo na aliyekuwa waziri wake wa masuala ya vijana, Charles Ble Goude kuachiwa huru.

Kiongozi huyo wa zamani ambaye amekuwa katika jela za ICC kwa miaka saba, alikuwa rais wa Ivory Coast kati ya mwaka 2000 hadi 2011.

Alifikishwa katika mahakama hiyo kwa mashitaka ya uhalifu dhidi ya binadamu baada ya ghasia za baada ya uchaguzi kuzuka nchini mwake 2011 kufuatia kukataa matokeo ya kushindwa katika uchaguzi ambapo watu zaidi ya 3,000 waliuawa.

Waendesha mashitaka wa ICC wamesema wanapanga kukataa rufaa uamuzi huo wa majaji kumuachia huru Gbagbo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles