24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Dar ya kijani ya UVCCM yavuna wanachama 500

MWANDISHI WETU

NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Rodrick Mpogolo, amewapokea wanachama wapya wa chama hicho kupitia kampeni ya Dar ya kijani inayoratibiwa na Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Mkoa wa Dar es Salaam.

Kampeni hiyo ya Dar ya Kijani ina lengo la kurudisha mitaa, kata na majimbo yote katika himaya ya chama, inawataka vijana na wanachama wote kuimarisha ushirikiano na kupata ushindi wa pamoja wenye heshima kwa chama hicho tawala.

Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo kwa Wilaya ya Kinondoni, Mpogolo, amewataka vijana kuwa makini na waadilifu kwani wao ndio wataokaojenga heshima ya chama na Taifa kwa ujumla.

“Vijana ndio tunao wategemea katika uchaguzi ujao tunahitaji vijana makini na waadilifu ambao watakitumikia chama chetu cha Mapinduzi na Serikali yetu. jiepushieni mbali na tabia ambazo zitawaondelea maadili yenu. Ili mkawe viongozi makini kwani taifa letu linaitaji viongozi makini na wachapakazi .

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rodrick Mpogolo, akizungumza kwenye uzinduzi wa Dar ya Kijani

Amesema yeye hatoita Dar ya Kijani ila anaitambua Tanzania ya Kijani kutokana na kazi kubwa inayofanywa na serikali ya Chama Cha Mapinduzi ya kuwaletea Watanzania maendeleo ya kweli.

“Mimi sitaita Dar es Salaam ya Kijani bali nitaita Tanzania ya Kijani kwa sababu Rais wetu mpendwa Dk. John Magufuli anafanya kazi kubwa ya kuleta maendeleo nchini, tunaona ujenzi wa barabara za juu pale Ubungo na tunashuhudia maendeleo makubwa yanayofanywa katika sekta ya elimu vituo vya afya, kuwasaidia wamachinga kwa kuwapa vitambulisho vya ujasiriamali, bodaboda.

“Pia ameleta usawa kwa Watanzania*wote kuwa sawa. Kwahiyo kwa namna hii lazima chama chetu kiendelee kushika hatamu kwa sababu tunawatumikia wananchi ipasavyo kwa namna hii nina uhakika Tanzania inaenda kuwa ya kijani,” amesema Mpogolo

Kwa upande wake Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Dar es Salaam, Mussa Kilakala, amesema lengo la kampeni hiyo ya Dar es Salaam ya Kijani ni kuwaandaa vijana na chaguzi zijazo ikiwamo Serikali za Mitaa mwaka huu pamoja na Uchaguzi Mkuu mwaka 2020 ili chama hicho kipate ushindi wa kishindo.

“Lengo la Dar es salaam ya Kijani ni kuwaanda vijana wa Mkoa wa Dar es salaam katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa lakini kuwataka vijana kuhakikisha wanajitokeza katika kugombea nafasi lakini pia kuhakikksha CCM kinapata ushindi wa kishindo kwa mkoa wote,” amesema Kilakala

Amesema tangu kampeni hiyo ilipozinduliwa Machi 17, mwaka huu jijini Dar es Salaam imefanikiwa kuvuna zaidi ya wanachama 500  ambao wamejiunga na chama hicho.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles