31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

ANC yashinda Uchaguzi Afrika Kusini

JOHANNESBURG, A.Kusini

CHAMA   tawala nchini hapa,  African National Congress (ANC), kimefanikiwa kurejea madarakani, lakini safari hii kikiwa kimepata asilimia ndogo ya kura ikilinganishwa na miaka ya nyuma.

 Kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa mjini hapa  ANC, imepata asilimia  58 ya kura zote kikifuatiwa na Chama cha  Democratic Alliance (DA) kilichopata asilimia  21 na chama cha tatu kikiwa ni cha l Economic Freedom Fighters (EFF), ambacho kimepata asilimia 11.

Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Uingereza BBC tatizo la mdororo wa kiuchumi na rushwa ndivyo  vilivyoshusha umaarufu wa chama hicho kikongwe cha ANC.

Akizungumza mara baada ya kutangazwa matokeo hayo kiongozi wa  ANC,  Cyril Ramaphosa,aliwataka wananchi kuungana na kujenga Afrika Kusini yenye umoja.

Mbali na kujenga nchi yenye umoja, kiongozi huyo alisema kuwa ushindi huo umeonesha kuwa wananchi wa taifa hilo bado wanaimani na  ANC tangu ilipoingia madarakani mwaka  1994.

“Na sasa tufanye kazi kwa pamoja, watu weusi, wazungu wanaume kwa wanawake, vijana na wazee kujenga Afrika Kusini yenye umoja ni jukumu letu sote, ” Rais  Ramaphosa aliwaambia wafuasi wake mjini Pretoria.

Alisema kwamba anaitaka Afrika Kusini ambayo sio ya kiubaguzi wa rangi, kijinsia,kidemokrasia na kimafanikio.

Mwandishi wa BBC,  Will Ross anasema kwamba hata hivyo ilikuwa ikifahamika  ANC haiwezi kupata idadi kubwa ya kura.

Alisema ingawa idadi ya wafuasi wake wamepungua lakini jambo hilo halikutokana na utendaji wake mbaya pengine walitaka kuwapa nafasi wengi wajaribu kutafuta  ufanisi katika kukabiliana na  kashfa za rushwa zinazoikabili ANC  na kutafuta maendeleo ya  kukabiliana na umasikini.

Mwandishi huyo alisema kuwa chama hicho kimepata asilimia  65 katika mabunge yote mawili  idadi ambayo imeporomoka ikilinganishwa na asilimia  73 kilichopata miaka mitano iliyopita.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles