27.5 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

TUCTA yampongeza Magufuli kurudisha kikotoo cha zamani

Ferdnanda  Mbamila, Dar es  Salaam

Shirikisho la Wafanyakazi  nchini (TUCTA),  limempongeza  Rais  Dk. John Magufuli kwa uamuzi wake wa kurudisha kikokotoo cha zamani kiendelee kutumika kwani kitaleta tija kwa wafanyakazi.

 Kabla ya Rais Magufuli kufikia uamuzi huo kanuni za Usimamizi wa Mifuko ya Jamii ziliondoa mfumo wa zamani wa kulipa asilimia 50 ya mafao kwa mkupuo na  inayobaki kulipwa taratibu abapo mabadiliko yalitaka mstaafu alipwe alipwe asilimia 25 kwa mkupuo asilimia 75 itolewe kama pensheni kwa kila mwezi kwa kipindi chote cha maisha ya mstaafu jambo lililozua mijadala mbalimbali kuhusu jkanuni hizo mpya.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamis Januari 3,  jijini Dar es Salaam Dk. Yahaya  Msigwa Naibu Katibu Mkuu TUCTA, Dk. Yahaya Msigwa amesema wanamshukuru na kumpongeza Rais Magufuli  kwa  kuiweka sheria hiyo  wazi  kwa wafanyakazi ambapo inatarajia kufikia  ukomo  mwaka  2023.

 “Rais  ameweka sheria hiyo ili  kuwapisha wadau  mbalimbali nchini  ili  waje na sheria  yenye tija  na inayolinda  maslahi ya wafanyakazi katika  mifuko ya hifadhi za jamii.

 “Awali  mifuko hiyo  ilikuwa mitano na baada ya kuunganishwa sasa ipo miwili na ilitokana  kubadilishwa kwa sheria hiyo, hivyo kwa namna moja imewarahisishia wadau  wa mifuko hiyo kutoka katika mkanganyiko ambao uliwaweka gizani , “ amesema Dk. Msigwa .

Dk Msigwa ameitaja mifuko miwili ya jamii  iliyopo baada ya kuunganishwa ni Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF ) na Mfuko wa Watumishi wa Sekta binafsi (NSSF).

 Aidha mifuko mitano iliyokuwepo awali ni Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Serikali Kuu (GEPF), Mfuko wa Pensheni kwa watumishi wa Serikali za Mitaa(LAPF), Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) na Mfuko wa Pensheni kwa Mashirika ya Umma na NSSF yenyewe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles