23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Makonda kuwasaka wasiona vitambulisho vya ujasiliamali

Na Brighiter Masaki

Mkuu waMkoa  wa  Dar es salaam, Paul Makonda ametangaza msakokwa wafanyabiashara wadogo wasiokuwa na vitambulisho vya ujasiliamali vilivyo anza kutolewa mapema mwanzoni mwa mwaka  huu.

Msako huo ni moja ya mkakati wa ukusanyaji mapato kupitia wafanyabiashara hao.

Paul Makonda amesema June3 mwaka huu ni marufuku kwa mfanyabiasharayoyote mdogo kujishughulisha na biashara ndani ya mkoa huo bila kuwa na kitambulisho maalumu cha utambuzi kilichotolewa na Rais Dk John Magufuli.

Sambamba na hilo,mkuu wa mkoa huyo amewasihi wafanyabiashara hao walipe kodi ili waongeze wastani wa pato la taifa kupitia kodi.

Aidha Makonda amewataka wafanyabiashara wasiopata vitambulisho lakini wanavigezo vya kuvipata wafike sehemu husika ikiwemo ofisi za wakuu wa mikoa ili kuvipata.

Amesema takwimu kubwa zinaonyesha kuwa idadi ya wafanyabiashara wasiokuwa na vitambulisho ni kubwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles